24 Julai 2020 - 15:26
Wazayuni wamebomoa nyumba zaidi ya 2,000 za Wapalestina katika mwaka 2019

Utawala haramu na dhalimu wa Kizayuni wa Israel ulibomoa nyumba zaidi ya 2,000 za Wapalestina katika mwaka uliopita wa 2019.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: mamlaka za utawala haramu wa Kizayuni zilitoa amri ya kubomolewa nyumba 2,241 za Wapalestina katika eneo la Naqb mnamo mwaka uliopita wa 2019.

Kwa mujibu wa Fars, bomoabomoa hiyo ya nyumba za Wapalestina ilifanywa ama na jeshi la polisi la utawala haramu wa Israel au kupitia mpango wa watu "kubomoa wenyewe nyumba zao".

Utawala ghasibu wa Kizayuni umekuwa ukibomoa nyumba za wananchi madhulumu wa Palestina na kuwalazimisha kuhama katika maeneo yao ili kuyapora maeneo hayo kwa ajili ya kuwajengea nyumba wazayuni na kuwapatia makazi pale walipowahamisha Wapalestina.

Utawala haramu na dhalimu wa Kizayuni umedhamiria kubadilisha muundo wa kijiografia na kidemografia wa maeneo ya Palestina na kuyapa sura ya Kizayuni ili kuweza kuwa na udhibiti kamili wa maeneo hayo unayoyapora na kuyaghusubu ya ardhi za Palestina.../

342/